Pages

Thursday, June 12, 2014

AUA MKE WAKE KWA KUMCHOMA KISU SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI

Mbeya .Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoani hapa akiwemo Mwanamke mmoja mkazi wa  kijiji cha Isangati Mbeya vijijini  aliyekufa baada ya  kumchomwa  kisu  na mume wake  huku akiwa amelala.

Akizungumzia  matukio hayo kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alimtaja mwanamke huyo kuwa ni Madawa Jaston (29)na kwamba tukio  hilo  lilitokea jana majira saa  5:00 asubuhi kijijini hapo.


Alisema kuwa mtuhumiwa kabla ya kutekeleza tukio hilo alimvamia na kisha kumchoma  kisu mke wake maeneo ya usoni,kichwani na miguuni huku  akiwa amelala ndani na kukimbilia kusikojulikana na chanzo cha mauaji hayo bado kinachunguzwa.

Msangi anatoa wito  kwa mtu yoyote ambaye mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hilo atoe taarifa katika mamlaka husika ili aweze kukamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Tukio lingine ni la watu wawili waliokufa papo hapo baada ya magari mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana na kisha kupinduka katika kijiji cha Itewe barabara kuu ya Mbeya Iringa .

Msangi aliwataja waliokufa  katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na  dereva wa roli  aina ya Mistubishi  lenye namba za usajili T.254 BFZ Fuso  Rashid Mfinanga (37) mkazi wa uyole  na Goden Katemu (60).

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira saa 1:30 jioni baada ya gari hilo aina ya Fuso lililokuwa likitokea uyole kuelekea njombe liligonga ubavuni gari lenye namba za usajili T 837 ATC aina ya Toyota Haice lililokuwa likitokea Chimala na kuelekea Mbeya jiji lilokuwa likiendeshwa na Mradi Chande (34) na kasha magari yote kupinduka.

Wakati huo huo motto mwenye umri wa mika mitatu aliyetambulika kwa jina la Joshua Shukrani mkazi wa ilemi alifariki dunia wakati anapelekwa hospitalini  baada ya kugongwa na gari lisilofahamika na dereva asiyefahamika.

Msangi alisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 6:15 mchana katika eneo la mtaa wa mwafute  barabara ya Transfoma jijini Mbeya na kwamba chanzo cha ajali kinachunguzwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya.

                                                                 

0 comments: