Pages

Thursday, June 12, 2014

WAKALA WA VIPIMO MKOA WA MBEYA WAFANYA MKUTANO NA WADAU WA VIPIMO

 Kaimu meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya Deogratius Hussein akitoa taarifa mbele ya mgeni rasmi Kaimu katimu tawala Mkoa wa Mbeya Leonard Magacha katika ukumbi wa Goden City Hotel
 Wadau wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya wakiendelea na mkutano katika ukumbi wa Goden City Hotel
Kaimu katibu tawala Mkoa wa Mbeya (RAS)Leonard Magacha akitoa hotuiba yake katika mkutano wa wadau wa wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya.


Mbeya.Wakala wa vipimo (WMA)ametakiwa kujiimarisha  kwakufanya ukaguzi wa  mara kwa mara katika maeneo ya masoko ili kuweza  kutatua tatizo la Lumbesa linalosababisha wananchi na wakulima kudhurumiwa mazao yao.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu katibu tawala  Mkoa wa Mbeya Leonard  Magacha katika mkutano wa pamoja wa wadau wa  wakala wa vipimo uliofanyika katika ukumbi  Mbeya  Gorden City  jijini hapa.


 Magacha alisema kuwa  suala la Lumbesa bado ni tatizo kubwa linalowasumbua wakulima ambapo  wachuuzi wamekuwa wakijinufaisha kupitia lumbesa na kuwaacha Wakulima kuendelea kuwa masikini kutokana na kushindwa kupata faida ya mazao yao.

“Tunahitaji kuwa na ukaguzi wa kushitukiza wa mara kwa mara katika maeneo ya masoko yetu ili tuweze kumaliza tatizo hili ,shirikianeni na serikali za vijiji na kata pamoja na maafisa biashara wa Wilaya kwani peke yenu hamuwezi kufanikiwa katika kuondoa kero hii”alisema

Alisema kuwa mkoa wa Mbeya ni mkubwa na utaratibu unaotumika katika biashara ya bidhaa siyo vipimo halisi kwani uchunguzi unaonyesha ni asilimia moja ya Mkoa mzima ndiyo  wanatumia vipimo halisi.

Awali akitoa taarifa kaimu meneja wa Wakala wa vipimo Mkoa wa Mbeya Deogratias Hussein alisema kuwa wanakabilina na changaoto kubwa ya sheria kupita na wakati ambao adhabu zinazotolewa kwa mkiukwaji wa vipimo ni ndogo na hivyo kushindwa kumaliza tatizo la utumiaji wa vipimo visivyo halali hasa lumbesa.

Alisema kuwa Katika sheria ya vipimo  sura 340  iliyofanyiwa marekebisho 2002 inaeleza kuwa atakaye patikana na  hatia kutokana na kutumia vipimo visivyo halali adhabu yake ni  faini ya Sh10,000  kwa kosa la kwanza akirudia kosa basi atapewa adhabu ya kulipa faini isiyo zidi Sh20,000 au kifungo cha miaka isiyodizi mitatu jela.

0 comments: