Pages

Thursday, June 12, 2014

RIFT YA KWANZA MKOANI MBEYA YAZINDULIWA KATIKA JENGO LA CHAMA CHA WALIMU

Mmoja wa Walimu akiimbia shairi katika siku ya uzinduzi wa Rift ya Kwanza katika Mkoa wa Mbeya kwenye jengo  la ghorofa sita mali ya  chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoani Mbeya na ndiyo jengo lefu kuliko yote katika jiji la Mbeya 
 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza  katika uzinduzi wa Rift ya kwanza  Mkoani Mbeya katika jengo la  Ghorofa sita mali ya chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya


 Walimu wakicheza kwa furaha katika uzinduzi wa Rift hiyo




 Katibu wa chama cha Walimu Mkoa wa Mbeya (CWT)  Kasuku Bilago akitoa taarifa ya Mkoa


 Walimu wakiimba kwaya katika siku hiyo ya uzinduzi wa Rift
 Katibu Mkuu wa CWT   Yahya Msulwa akitoa hotuba katika uzinduzi huo
 Mgeni rasmi Kaimu katibu tawala  Mkoa wa Mbeya Nyasebwa akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo
Katibu Mkuu  wa chama cha Walimu Tanzania (CWT) Yahya Msulwa amesema kuwa chama hicho kinatarajia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwasaidia  Walimu katika kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Alitoa kauli hiyo jana mara baada ya uzinduzi wa Rift ya kwanza Katika mkoa wa Mbeya kwenye jengo jipya la chama hicho lenye  ghorofa Sita lililojengwa eneo la Soka matola  jijini hapa na kuwa ni  jengo pekee refu katika  jiji la Mbeya.

Alisema kuwa  mradi huo wa majengo ambao utajengwa katika mikoa yote hapa nchini utawasaidia Walimu kama dhamana na kuweza kupata fedha nyingi zinakazowekwa kwenye mfuko maalum utakoundwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya Walimu.

“Haya ni majengo ya walimu wote ambapo mwalimu mmoja mmoja atanufaika na majengo haya ambapo tayari mkakati umeandaliwa wa  kuunda mfuko maalum ambao utakuwa unatoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia katika kuboresha maisha yao’alisema

Alisema kuwa  kuhusu aunzishwaji wa benki ya Walimu tayari  kiasi cha Sh 16 bilioni  kimepatikana kwa ajili ya uwanzishwaji wa benki hiyo na kwamba baada ya miezi miwili kuanzia sasa inaweza kuanza kufanya kazi.

Msulwa alisema kuwa benki hiyo itakuwa ya biashara ambapo walimu na watu wengine watapata nafasi ya kupata mkopo na kwamba faida itakayopatikana benki itatoa gawio  na kurudi kwenye mfuko  huo maalum wa  kuwasaidia Walimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CWT Mko wa Mbeya  Mwl Nelusigwe Kajuni alisema kuwa lengo la kuweka rift  katika  jengo hilo ni kuwasaidia walimu wenye ulemavu kufika kwa urahisi katika ofis husika na kuwez a kupata huduma  wanazozihitaji.

Mwl Kajuni  alisema kuwa malengo mengine ni kuongeza tija  na ufanisi wa kazi kwa watendaji wa CWT na kwa jamii nzima inayowazunguka na kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati.

0 comments: