Pages

Saturday, May 31, 2014

MGANGA ANAYEUNGANISHA MIFUPA YA BINADAMU KWA DAWA ZA MITI SHAMBA NA WANYAMA



Pichani  ni mgonjwa  Wordson Pakyindi akitembea kwa kutumia magongo mara baada ya kuunganishwa mifupa kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu ,nyuma yake ni mganga wa asili aliyemtibu Anyimike Mabeja  katika kijiji cha Bwenda Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.



Pichani  ni mganga wa asili anayeunganisha mifupa kwa kutumia  dawa za miti shamba na Wanyama  Anyimike Mabeja akimwangalia mgonjwa wake Wordson Pakyindi sehemu ambayo amemuunganisha mifupa kwa kutumia dawa hizo   katika kijiji cha Bwenda Wilaya hya Ileje Mkoani Mbeya.



Pichani  ni mgonjwa  Wordson Pakyindi akitembea kwa kutumia magongo mara baada ya kuunganishwa mifupa kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama baada ya kupata ajali na kuvunjika mguu ,nyuma yake ni mganga wa asili aliyemtibu Anyimike Mabeja  katika kijiji cha Bwenda Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.

Ajali za barabarani, vipigo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikichangia watu wengi kupata ulemavu wa kudumu na wengine kulazimika kuondolewa kabisa viungo vyao kwa kuvikata kutokana na kuonekana kitaalamu havitaweza kutibika tena.

Tishio la kupata ulemavu limekuwa likitia hofu watu wengi kutokana na ukweli kuwa pindi mtu anapopata ulemavu, uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi unapungua kwa kiasi kikubwa na mtu kuanza kulazimika kwa kiwango fulani kuwa tegemezi.

Licha ya kuwepo kwa Hospital na madaktari bingwa bado matumaini ya wananchi kupona yamekuwa ni madogo kutokana na kukithiri kwa madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa na hivyo kuwa kikwazo kwa watu wa kawaida kupata tiba katika Hospitali zetu.
Lakini wakati wananchi wakikabiliwa na changamoto mbalimali za kupata huduma katika Hospitali nchini, huenda tumaini jipya likawa limepatikana kutokana na kuibuka kwa mtaalamu wa tiba mbadala ya kuunganisha mifupa na kutibu majeraha kwa kutumia dawa za miti shamba na wanyama.

Huyu ni si mwingine ni Anyimike Malabeja(56)mkazi wa kitongoji cha Mtambo kijiji cha Bwenda  kata ya lubanda wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya umbali wa kilometa 50 kutoka barabara kuu ya kutoka Mbeya mjini  kwenda Nchini  Malawi ambaye anatoa tiba ya kuunganisha mifupa na kutibu majeraha kwa kutumia dawa za miti shamba na Wanyama.

Mabeja ni  mtoto wa sita katika familia ya mzee Patisi Mabeja anasema kuwa alianza kutoa tiba hiyo baada ya kurithi kutoka kwa baba yake ambaye pia kazi hiyo alirithi  kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa akitoa tiba hiyo wakati wa ukoloni kutokana na mazingira waliyokuwa wakiishi kutokuwa na hospitali na wataalam wa dawa za kisasa kwa ajli ya kutoa tiba hiyo mara wanapokuwa wamepatwa na matatizo ya kuvunjika mifupa.

“Huu utaalam ni kutoka kwa mababu zetu alianza kufanya babu yake baba akaja baba yake baba  na baadae akaja baba yangu ambaye ndiye aliyenirithisha mimi kutokana na hali ya  baba kwa sasa hajiwezi anaumri  zaidi ya miaka 90”anasema

Anasema kuwa baba yake mzazi alianza kutoa tiba hiyo mwaka 1982 ambapo watu wengi wa kutoka vijiji mbali mbali wamekuwa wakipata tiba kutoka kwa huyo baba na wamekuwa wakipona huku akiwa anajifunza na kwamba baba yake huyo aliweza kumshirikisha kwa ukaribu na kutoa maelekezo jinsi dawa hiyo inavyotibu na inavyopatikana.

Dawa inayotumika katika kutoa tiba hiyo 

Mabeja anaeleza aina ya dawa inayotumika katika kutoa tiba hiyo kuwa ni mizizi , majani na wanyama ambapo mizizi inaitwa Mlumila kwa Lugha ya Kindali na upande wa majani dawa hiyo inaitwa Nalutete na Nakisokoso.

Anasema kuwa shughuli za kuunganisha mifupa zinaendana tiba ya kansa hivyo na kuwalazimu kutumia dawa ya ugonjwa wa  Kansa pamoja na dawa hizo katika kutoa tiba ambapo dawa hiyo ya kansa inatokana na Wanyama   ambao ni Kapenka(Panya buku),jamii ya nyani wenye rangi nyeupe(Mbega)na mdudu ambaye anapenda kukaa kwenye matope(Kabhwa kabhwa).

Mabeja anaeleza kuwa dawa hizo zinapatikana polini  ambapo kuna umbali mrefu una kulazimika kutumia siku mbili hadi tatu kwenda kurudi nyumbani kwake kutokana na mazingira ya kijijini yalivyo hivyo ulazimika kutembea kwa mguu kwa siku hizo .

Jinsi anavyofanya kazi ya kutoa tiba hiyo

“Ninaotaalam wa kugundua tatizo hata bila kutumia picha kama wanavyofanya hospitalini hivyo ninauwezo kugundua ni aina gani ya mfupa ambao umevunjika na jinsi ya  kupunguza mfupa na kuupanga vizuri” hunichukua nyumbani

Anasema kuwa kuna mifupa ambayo inatoka nje na mingine ipo ndani kwa ndani ambapo  hutumia utaalam aliofundishwa na babu zake  jinsi ya kutambua  tatizo na jinsi ya kulitibu na mgonjwa anapona kwa kutumia  dawa ya ganzi ya hospitalini.

Anafafanua kuwa mara baada ya wagonjwa kumaliza matibabu kwake  huwa anawashauri kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kujiridhisha kama amepona “wengi wamefanya hivyo na wamekuwa wakipona kabisa”anasema

Anasema kuwa amekuwa akiwapokea wagonjwa  ambao wameshindwa kupata tiba kutoka kwenye hospitali mbali mbali ikiwa ni pamoja na rufaa Mbeya  ambao wanakuwa na taarifa ya  uwepo wake  na wengine humchukua nyumbani kwake na kwenda kutoa tiba kwa wagonjwa ambao wana hali mbaya na  hawana uwezo wa kutembea.

Mganga huyo anasema kuwa enzi za mababu mawahgonjwa walikuwa wanatoa mbuzi mmoja kama gharama ya matibabu lakini kwa sasa wanatoa shilingi 70,000 pekee ambayo ndiyo gharama ya mbuzi mmoja kwa  wakati huu.

Anasema kuwa amekuwa akipata ushirikiano kutoka kwa serikali ya kijiji,kata na hospitali teule ya Wilaya ya Ileje ia Isoko ambapo humsaidia kupata vifaa vya kuvaa mkononi(Gloves) wakati wa kutoa tiba na dawa ya ganzi .

Changamoto anazokumbana nazo katika kutoa tiba hiyo

Mabeja  anaeleza changamoto anazokutana nazo ikiwa ni pamoja ukosefu wa usafiri kwa ajili ya kwenda kutafuta dawa,ukosefu wa mawasiliano hapo kijijini kwake na hivyo kushindwa kuwasiliana na wagonjwa wake .

“Huku kwetu hakuna mawasiliano kama unavyokuona mazingira yake hivyo nashindwa kabisa kuwasiliana na wagonjwa wangu kwani nimeweza kuwahudumia wagonjwa kutoka ndani ya mkoa na nje kama vile Mkoa wa Morogoro na iringa ambako nimekwenda kutoa huduma na huwa na tibu wagonjwa 20 kwa mwezi”anasema

Kauli ya mgonjwa aliyepata tiba hiyo

Mkazi wa kijiji cha  Kyimo Wilaya ya Rungwe Wordson Pakyindi(30)ni mgonjwa ambaye amepatiwa tiba na mganga huyo mara baada ya kupata ajali ya pikipiki na kuvunjika mguu naeleza jinsi alivyopata tiba kutoka kwa mganga huyo.

Anasema kuwa alipata ajali ya pikipiki baada ya kugongwa na gari aiana ya Toyota Hiace Desemba 17,2013 katika eneo la  Igawilo uyole jijini Mbeya akiwa anakwenda kazini kusababisha kuvunjika mguu wa kushoto na paja kupasuka na kusababisha kuwepo kwa kidonda kikubwa ikiwa ni pamoja na goti kuhama katika sehemu yake.

“Baada ya ajali hiyo wasamalia wema walinibena ma kunipeleka katika hospitali ya rufaa mbeya ambpo nilipatiwa huduma ya kwanza kwa nishona sehe,u ya paja iliyokuwa na kidonda na wakati napelekwa kwenye chumba cha kupigwa picha (x-ray)nilifuatwa muuguzi aliyekuwa ananihudumia na kuniambia kuwa wenzio wanokuja hapa huwa wanatoa fedha ndipo wanahudumiwa vizuri kauli hiyo iliniongezea maumivu”anasema

Anasema kuwa baada ya kupiga picha hiyo alipelekwa wodini  ambapo madaktari walimwambia  kuwa    anatakiwa kuwekwa chuma bila ganzi kutokana shinikizo la damu kuwa chini (BP Kushuka)”hali ambayo nilikataa kuwa siwezi kuwekwa chuma bila kutokana na maumivu makali niliyokuwa nayapata wakati ule”anasema

“Niliwaeleza ndugu zangu kuwa sipo tayari kuwekwa chuma bila ganzi na ndipo alipokuja kaka yangu na kuniambia kuwa huku kuna mganga ambaye angeweza kunitibu na nikapona hivyo nilimkubalia kuja huku kwani nili kuwa siwezi kuinuka,kukaa wala kugeuka zaidi ya kulala pekee”anasema

Anasema kuwa waliondoka hospitalini hapo kwa kuwaeleza wauguzi kuwa wameamua kwenda hospitali ya mission Peramiho Mkoa Ruvuma na  kufanikiwa kuruhusiwa kuondoka hospitalini hapo siku ya pili mara baada ya ajali.

“Nilipokuwa natoka rufaa hali yangu ilikuwa mbaya  kwani huduma niliyokuwa nimepa ni ya kushonwa kidonda  ili kisiendelee kutoka damu nilikuwa siwezi kutembea wala kutikisika nilikuwa nabebwa kama jiwe lakini namshukuru mungu mara baada ya kufika hapa hali yangu ni nzuri kwa sasa naweza hata kuinuka peke yangu na kuchukua magongo yangu na kuanza kutoka nje”anasema

Anasema kuwa mara baada ya kufika hapo mganga huyo aliweza kuunganisha  mfupa bila ya kuwekwa chuma na goti kulirudisha sehemu yake na kwamba kkwa sasa kidonda kimepona kilichobaki ni goti ambalo limesababisha atumie msaada wa  magongo katika kutembea.

“Namshukuru sana huyu mganga kwani ameokoa maisha yangu kwani ningeweza kupata ulemabu wa maisha lakini amenitibu vizuri na nimeridhika kama unavyoniona hapa na muda siyo mrefu nitarudi nyumbani  na kuendelea na kazi zangu najiona nimepona ni hili goti ndiyo bado kidogo kupona “anasema

Mgonjwa huyo ameiomba serikali  kuwa karibu na mganga huyo ili kuweza kumuwezesha katika kutoa tiba yake na kuweza kuwasaidia wagonjwa hasa wale ambao wanakuwa hawana uwezo wa kumudu gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitozwa katika hospitali kubwa zenye uwezo wa kutibu magonjwa kama hayo.

“Serikali isiangalie waganga wale wanaojitangaza kwa mabango makubwa  na kwenye vyombo vya habari  mganga wa ukweli hajitangazi bali anafuatwa hivyo ni vema wakamtumia huyu mganga kwa ajili ya kuokoa nguvu kazi  kubwa ambayo imekuwa ikipotea kutokana na baadhi ya watu kuwa na ulemavu wa maisha kwa kukatwa miguu”anasema

Naye Abduwnuwasi Kalinga mkazi wa kijiji cha Bwenda anasema kuwa mganga huyo amekuwa ni msaada mkubwa katika eneo hilo watu wengi wamekuwa wakipata ajali katika shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kucheza mpira na kuanguka kwenye mti.

“Tumeshuhudia watu wengi ambao wamefika kwa mganga huyu na wamepona na kwa hapa kwetu kijijini vijana wengi wamehudumiwa na huyu mganga na wamepona bila hata ya kwenda hospitali kama unavyojua kutoka hapa kwenda hospitalini ni mbali  sana na usafiri hakuna hivyo wote tunamtegemea huyu mganga kwa ajili ya kupata tiba hapa”anasema

anasema kuwa tatizo siyo serikali bali ni watoa huduma katika hospitali kuwaona wagonjwa kwa kutanguliza masilahi yao binafsi badala ya kutoa huduma kwanza na hivyo kusababisha watu masikini kupata ulemavu wakudumu kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Ileje Sylivia Siliwa anasema kuwa mganga huyo wanamfahamu na wagonjwa wengi wamepona kupitia tiba yake ila bado hajajisajili na kuweza kutambulika  kama waganga wengine wa tiba ya asili.

“Nimemsikia na halmshauri yetu inafahamu kuwepo kwa mganga huyu lakini bado hajajisajili kwani anatakiwa kujisajili na kujiunga na umoja wa waganga wa tiba ya asili ili aweze kupata  kibali na  kuweza kutambulika  kisheria”anasema

Anasema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni mganga huyo kuanza utaratibu wa kuhakikisha anajiunga na umoja huo ambao utamsaidia kutambulika kishera na kuweza kupata msaada wa aina yoyote ambao anauhitaji  kutoka halmashauri  na kuweza kutoa tiba yake vizuri na kwa watu wengi.

 

0 comments: