Pages

Thursday, February 6, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika moja ya miradi ya maendeleo katika kijiji cha Mshewe halmshauri ya Wilaya ya Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amebaini madudu katika halmashauri  ya Wilaya ya Mbeya baada ya  Sh 208 milioni kutolewa  kwenye kikundi kisicho halali (kikundi  hewa)  na kati ya hizo Sh21milioni zikiwa zimetumika  katika kijiji cha Imezu  kata ya Itewe  Wilayani humo.
 
Kandoro alibaini hayo juzi alipotembelea kijiji hicho ambapo kuna ujenzi wa mradi   wa mfereji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ulioibuliwa na wananchi  unaotarajia kugharimu kiasi cha Sh 208 milioni hadi kukamilika kwake.


Akitoa maelezo  ya mradi huo  Diwani wa kata ya   Inyala Kisemba Mwalingo alisema kuwa awali kulikuwa na kikundi kilichodai kuwa kinatoka katika kijiji hicho  ambacho kiliwasilisha andiko la kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo  na kupewa kiasi cha Sh108 milioni.

Alisema kuwa baada ya fedha hizo kuingia kwenye akunti ya kikundi hicho wahusika walianza kutumia fedha hizo  ambpo awamu ya kwanza walichukua Sh10milioni na awamu ya pili walichukua Sh 11milioni huku  mkandarasi akiwa hajatafutwa.

“Mara baada ya kuchukuliwa fedha hizo ndipo ilipobainika kuwa  kikundi hicho  siyo halali na hakitambuliki hapa kijijini  kutokana na wananchi kueleza kuwa watu hao siyo wenyeji katika kijiji hicho”alisema 

Alisema kuwa  baada ya kufuatilia  na kufanya uchunguzi wa kina ilibainika kuwa kikundi hicho ni cha mtu mmoja  na ndipo Mkurugenzi alipochukua hatua za kuzuia akunti hiyo isitoe fedha zingine “wakati tayari walikuwa wameshatoa  fedha  jumla ya Sh21milioni”alisema 

Kwa upande wake Kandoro alimwagiza kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya  kumfikishia wale wote waliohusika utoaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja  na kuwataka kurudisha fedha hizo za seerikali ambazo zililetwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi.

0 comments: