Pages

Tuesday, September 2, 2014

JESHI LA POLISI LAZIMA MAANDAMANO YA WAUMINI ZAIDI YA 500 WA KANISA LA MORAVIAN MBEYA

Mbeya.Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya, limezuia  maandamano ya  waumini zaidi ya 500 wa   Kanisa la Moravian jimbo la kusini Magharibi, yaliyotakiwa kufanyika leo,  ya kushinikiza kufanyika mkutano wa dharula wa Sinodi  kwa lengo la kumaliza mgogoro wao uliodumu   kwa mwaka mmoja na nusu.

Kanisa la Moraviani  jimbo lakusini magharaibi  limekuwa na mgogoro uliodumu zaidi ya mwaka mmoja . mara baada kumvua  madaraka  Mwenyekiti wa jimbo  hilo Nosigwe Buya   na  kusimamishwa kazi wachungaji watano waliodaiwa kuhusika kumtetea mwenyekiti huyo.

Akizungumza na  gazeti hili Mwenyekiti wa waumini hao Frank Phiri alisema kuwa leo walipanga kufanya maandamano ya amani kwa lengo la kushinikiza kufanyika kuitishwa mkutano wa Sinodi baada ya kuona viongozi wa kanisa hilo hawafuati maamuzi  na maagizo ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama  Wilaya ya Mbeya.

“ Tulifiata taratibu zote za kuomba kibali cha kufanya maandamano na tayari waumini kutoka  Wilaya zingine walishaingia tangu  lakini cha kushangaza polisiwamtuzuia kufanya hivyo kwa madai kuwa wanahofu vurugu zinaweza kutokea  kitu ambacho tunaamini sisi kuwa siyo  cha ukweli”alisema

Alisema kuwa  juzi siku ya ijumaa waliwasilisha barua ya kuomba kibali  katika ofisi wa mkuu wa polisi wa Wilaya ya Mbeya (OCD ) ambaye alikiri kuipokea na kuwataka warudi jumamosi ambapo walipofika  ofisini kwake walimkuta OCD huyo akiwa na katibu mkuu wa  jimbo hilo.

“Hali  hii inatufanya tukose imani na serikali yetu kwani  kama  viongozi  wa kanisa wameshindwa kufuata maaagizo na maamuzi  ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya  ya kumrudisha  Mwenyekiti katika nafasi yake  na badala yake wanachukua uwamuzi mwingine wa kuwafukuza wachungaji watano  sasa sisi waumini  wanataka tuwe upande gani”alisema 

Alisema kuwa kama waumini wanaamini kuwa  mkutano wa  dharula wa Sinodi  ndiyo unaweza  kumaliza mgogoro huo na kuliweka kanisa  pamoja kama katiba inavyoeleza  ‘lakini hawa wenzetu viongozi hawataki kuitisha Sinodi  wakatgi ndiyo iliyowaweka  madarakani  kufanya hivyo ni kuliua kanisa  kwani mgogoro huu hauwezi kuisha bila ya kuitishwa kwa mkutano huu.”alisema

Akieleza sababu za  kuzuia  maandamano hayo  kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya  Ahmed Msangi alisema kuwa wamefanya hivyo baada ya uchunguzi  wao kubaini kuwa  maandamano hayo yanaweza kuleta machafuko kutokana na mgopgolo ulivyo.

“Kweli tumezuia kufanyika  kwa maandamano hayo kwani kila upande kuna mambo wanataka kufanya mara huyu anataka hili,huyo mwingine anataka hili hivyo tumeona ni vema tuwakatilie wote  ili kuepusha machafuko ambayo yangeweza kutokea”alisema

0 comments: