Pages

Wednesday, September 3, 2014

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LAKARABATI MADARASA

 MSTAHIKI Meya wa jiji .la Mbeya Atanas akizungumza katika hafla ya kuzindua vyumba vya madarasa vinne na jengo la Utawala katika shule ya msingi Hassanga  Uyole jijini hapa  baada kufanyiwa ukarabati na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliogharimu  Sh.31.5milioni.


 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Prof..Norman Sigallah King akimkaribisha mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi waliohudhulia hafla hiyo
 Mkuu wa Mmoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa ameshika Boksi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufanyia ukakarabati wa madarasa mengine manne katika shule hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh 2.3milioni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi waliohudhulia hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC  Nehemiah Mchechu akizungumza katika hafla hiyo
 Mwalimu Neema Sanga akisoma taarifa ya shule ya msingi ya Hassanga
 Wanafunzi wa shule ya msingi Hassanga wakiimba kwaya  katika hafla hiyo

 Mmoja wa Wanafunzi wa shule ya msingi hassanga  akiimba Ngonjera

  Mkuu wa Mmoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa ameshika Boksi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kufanyia ukakarabati wa madarasa mengine manne katika shule hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh 2.3milioni kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi waliohudhulia hafla hiyo.





Mbeya.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jana limekabidhi  vyumba vya madarasa vinne na jengo la utawala  kwa shule ya  msingi Hassanga jijini Mbeya  baada ya kuyafanyia  ukarabati   uliogharimu  Sh 31.5 milioni.

Akitoa taarifa ya matengenezo ya  shule hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  Mkurugenzi wa  mkuu wa NHC Nehemiah Mchechu  alisema kuwa   uwamuzi wa  kufanya ukarabati huo  ulitokana na maombi yaliyofanywa na kamti ya uongozi wa shule kwa kupitia afisa elimu Wilaya yaliyopelekwa   ofisi za NHC Mbeya  Februari mwaka huu.

Alisema kuwa  kazi hiyo ilianza Aprili 19 na kumalizika  Agosti 20 mwaka huu  ambapo jumla ya Sh. 22.7 milioni zitumika katika ukarabati wa jingo la utawala  na  Sh.8.8 zilitumika katika kukarabati wa maradasa manne.

Mchechu alisema kuwa baada ya  kufika shuleni hapo na kujionea ubovu wa  vyumba vingine vya madarasa hivyo shirika  hilo pia lipo tayari kumalizia madarasa mengine manne ambappo ujenziu huo utaanza rasmi kesho.

Akizungumza wakati wa kupokea madarasa hayo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alisema kuwa wananchi na serikali wanapaswa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shirika hilo katika shughuli za maendeleo.

“Ni lazima tuwashukuru hawa ndugu zetu lakini pia tunakila sanbabu ya kuwaunga mkono hivyo naanzisha harambee ndogo hapa ambapo kila mmoja achangia alichonacho ili tuweze kuzikabidhi  kwa mkurugenzi wa NHC kwa ajioli ya kutumalizia madarasa yetu mengine  manne yaliyobaki”alisema

Akitoa taarifa  kwa niaba ya  uongozi wa shule Mwalimu Neema Sanga alisema kuwa shule hiyo inajumla ya vyumba vya  madarasa 14 ambapo vine vipo katika hali nzuri baada ya kukarabatiwa NHC huku vilivyobaki vikiwa na hali mbaya.

Alisema bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa madawati 150  na ukosefu wa uzio  kwa ajioli ya ulinzi na usalama wa mali za shule.

Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya abasi Kandoro wakati kukabidhi madarasa hayo zaidi ya Sh2.3 zilipatikana kwa ajioli kuchangia ukakarabati wa  vyumba vingine vine vya madarasa

0 comments: