Pages

Tuesday, December 10, 2013

AMREF yawapiga msasa Waandishi na Wahariri Morogoro








Shirika la utafiti wa madawa na tiba (AMREF) limetoa  mafunzo  ya haki za afya  ya uzazi kwa vijana kwa baadhi ya Waandishi wa habari  na  Wahariri nchini ili kuwajengea uwezo wa    kuandika kwa undani  habari za afya ya uzazi na kuibua changamoto zake katika jamii .

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika  katika chuo cha kilimo  SUA  na kushirikisha waandishi  22 kutoka katika mikoa ya Njombe,Iringa,Mbeya,Morogoro na   dar es  Salaam ambapo pia waraweza kujifunza uandishi wa  habari za kiuchunguzi na maadili ya uandishi wa habari za afya ya uzazi kwa vijana.


Kwa mujibu wa mchambuzi wa sera na mwezeshaji wa mafunzo hayo  kutoka AMREF  Meshack Mollel malengo  ya mafunzo hayo kuwezesha waandishi kuwa na uwelewa kuhusu afya ya uzazi  kwa vijana na kuweza kuandika kwa undani habari za afya ya uzazi kwa vijana.

 Mollel alisema kuwa AMREF inatekeleza mradi wa haki za  afya ya uzazi kwa vijana katika kipindi cha miaka mitatu kwa Wilaya tatu za Ilala na Kinondoni  kwa mkoa wa Dar es Salaam na Manspaa ya Iringa.

“Kutokana na kuwepo kwa mradi shirika likaona ni vema likatambua umhimu wa waandishi wa habari kupata  mafunzo haya na kuweza kushirikiana na shirika katika kuandika habari kwa undani za afya ya uzazi kwa vijana na kwenda vijijini kubua changamoto  kwa jamii”alisema 

Alisema kuwa katika mradi AMREF imelenga kuwafikia 100,000 katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 na kwa vijana 100 wenye ulemavu wa kusikia wenye umri wa kuanzia miaka 10 hadi 24.

Mollel alisema kuwa katika mradi huo tayari vituo viwili vimeanzishwa kwa ajili ya vijana kwa ajili ya kutoa afya ya uzazi kwa vijana  ambapo vijana wanapata nafasi ya kuelimishwa na kupata tiba ya afya ya uzazi na kwamba kuna maeneo makuu  ya mradi ambayo ni pamoja na huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana,utetezi na sera ya afya ya uzazi kwa vijana na kujenga uwezo kwa watoa huduma.

0 comments: