Pages

Thursday, December 12, 2013

Utoaji wa elimu ya afya kwa vijana ni tatizo kwa familia za kiafrika

 Washiriki na mafunzo ya haki za afya ya uzazi kwa vijana wakifanya kazi za vikundi yaliyoandaliwa na  shirika la AMREF na kufanyika katika  chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Morogoro

 Imeelezwa  kuwa  wazazi na familia za Kiafrika hawana utaratibu wa kutoa elimu ya afya kwa watoto wao walio na umri  kuanzia miaka 10 hadi 16 kwa madai kuwa watakuwa wamechangia  watoto hao  kujiingiza katika  mahusiano ya kimapenzi.

Hayo yamebainika katika kituo cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Morogoro(WAVUMO)waliokuwa wakizungumza na waandishi wa habari waliopo katika mafunzo ya haki  za afya ya uzazi kwa vijana yaliyoandaliwa na shirika la utafiti wa madawa na Tiba (AMREF)  walipotembelea kituo hicho.


Akizungumzia tatizo hilo muuguzi wa kituo hicho Monica Kayembele alisema kuwa tamaduni na mira za kiafrika wazazi wengi hawana utamaduni wa kutoa elimu ya uzazi kwa watoto wao kwa imani kuwa watakuwa wanashiriki kuchangia watoto wao kujiingiza katika  mahusiano ya kiimapenzi.

Alisema kuwa mara kadhaa  kituo hicho kimekuwa kikipokea watoto ambao wamekuwa wakiletwa na wazazi wao kwa malengo ya kupewa elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na kuambukizwa na wazazi wao.
“Kutokana  mila wazazi wengi kuongelea masuala ya uzazi wamekuwa hawapo wazi hivyo kusababisha masuala ya maambukizi na mimba za utotoni kuendelea kujitokeza”alisema

Kwa upande wake mratibu wa kituo hicho Sara Mokiwa alisema kuwa kituo hicho pia kimekuwa kikipokea watoto ambao  walipata maambukizi kutokana na vitendo vya ubakaji na wengine kwa kujiingiza katika masuala ngono wakiwa katika umri mdogo.

Aidha alisema kuwa kituo hicho kinahudumia watu 3267 wakiwepo watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 14  idadi yao 156,umri kati ya 15 hadi 17 watoto 27 na unri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea wakiwa 3081.

Kwa upande wake mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sikujua John mkazi wa kikundi  alisema kuwa mila na tamaduni zilizozoeleka tangu enzi za mababu ni mwiko kwa mzazi kumweleza mtoto ambaye bado ahajakua masuala ya afya ya uzazi.

“Unajua waandishi kitu hiki nikigumu na hakiwezekani kwani hata sisi wakati tunakua wazazi wetu walikuwa wakitudanganya kuwa wananunua watoto dukani na siyo kwamba mama amejifungua mtoto na ndivyo tulivyoa amini kuwa watoto wananunuliwa dukani “alisema

Naye mtoto Joseph Januari mwenye umri wa miaka 12  mkazi wa  mtaa wa uhuru alipohojiwa kama amewahi kupata taarifa yoyote kuhusu afya ya uzazi alisema kuwa hajawahi kusikia zaidi ya kusikiliza matangazo ya television na radio.

0 comments: