Pages

Wednesday, December 18, 2013

Madiwani Wanne wa Chadema wahojiwa na polisi



MADIWANI   wanne kati  ya  18 chama cha Demkrasia na maendeleo   Chadema na NCCR Mageuzi  katika Jiji la Mbeya  juzi walihojiwa  na   jeshi la polisi Mkoani hapa  kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.

Juzi Madiwani 18 wa chama cha Demkrasia na maendeleo   Chadema na NCCR Mageuzi  katika Jiji la Mbeya walipata taarifa  kwa njia ya simu kwa ajili ya   kuhojiwa na jeshi la polisi Mkoani hapa  kwa tuhuma za kughushi majina ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga.


 Kwa mujibu wa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Mbeya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwakibete, Lucas Mwampiki  madiwani  waliohojiwa ni pamoja na Uswege Furika  diwani wa kata ya Ilemi, Deogratius Kapusi Diwani wa kata ya mbalizi Road na madiwani wa viti maalum Esther Mpwiriza na Sarah Kitumbula 

Mwampiki alisema   jana walipigiwa simu za kuitwa kuhojiwa na jeshi la polisi ambapo madiwani 12 ndiyo waliofika katika ofisi ya RPC ambako ndiko mahojiano hayo yalifanyika lakini kutokana na muda walkihojiwa madiwani wanne pekee.

“Kutokana na muda walifanikiwa kuwahoji madiwani wanne na kutuambia sisi wengine  tuondoke watatuita  siku nyingine kwa ajili ya kufanya mahojiano hayo “alisema 

Akizungumza na Blog hii Diwani wa kata ya Forest  ambaye pia ni kiongo
zi wa madiwani wa upinzani katika halmashauri ya jiji la Mbeya  Boyd Mwabulanga kuhusu tuhuma za saini yake kugushiwa  alisema kuwa yeye ndiy aliyeruhusu jina lake liandikwe na kusainiwa kwani maamuzi hayo yalikuwa ya pamoja na siyo ya madiwani wachache.

“Aliyepaswa kulalamika kuwa saini yake imegushiwa ni mimi na siyo halmshauri au Mkurugenzi hayo yalikuwa ni makubaliano ya sisdi madiwani wa upinzani na tulikubaliana kuwa barua ya kuomba mkutano maalum iandikwe na mimi na mbunge tukabariki majina yetu yaingizwa kwenye orodha hiyo sasa iweje walalamike wao kama halmashauri”alihoji

Diwani huyo ambaye yupo jijini dare s Salaam kwa ajili ya matibabu  alisema kuwa kitendo hicho cha kuwashitaki madiwani hao  ni mbinu za baadhi ya viongozi wa  halmashauri  ya jiji la Mbeya kutaka kuficha ukweli na kuzuia hoja za madiwani wa upinzani kutojadiliwa katika  kikao cha baraza la madiwani kama kanuni zinavyoelekeza.

Hivi karibuni baraza la madiwani liliazimia kuwachukulia hatua za kisheria madiwani wa upinzani  kwa tuhuma za kughushi sahihi za mbunge na diwani wakati wa kuorodhesha majina ya madiwani waliotaka kuitishwa kwa kikao cha dharura wa kujadili kutofuatwa kwa ratiba ya vikao vya halmashauri na kuhitaji ufafanuzi wa  matumizi mabaya ya Shilingi milioni 95 zinazodaiwa kutumiwa na maofisa watano wa jiji walipotembelea nchini China, 

0 comments: