Pages

Friday, August 29, 2014

AJALI YA YAUA WATU 10 MBEYA AKIWEMO MAMA NA MTOTO WAKE

 Wakati wa mji mdogo wa Mbalizi  Wilaya ya Mbeya waangalia  gari iana Toyota Hiace lililogongana na roli aina ya Fuso na kusabnabisha watu 10 kufa papo hapo akiwemo mama na mtoto wake na wengine nane kujeruhiwa katika eneo lililo karibu na kituo cha mafuta barabara kuu ya kutoka Mbeya kwenda Tunduma.







Mbeya.Vilio na Simanzi vimetawala katika mji mdogo wa Mbaralizi Wilaya  ya Mbeya vijijini  baada ya Watu 10  kufa papo hapo akiwemo mama na mtoto wake, na wengine nane  kujeruhiwa baada ya  Toyota Hiace walioyokuwa kisafilia kugongana  na roli  katika  eneo lilokaribu na kituo cha Mafuta.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:00 mchana  imehusisha gari aiana ya Toyota Hiace  ailiyokuwa ikitokea Mwanjelwa kuelekea Mbalizi na kuigonga roli  aiana ya fuso lililokuwa litokea katika kituo cha mafuta na kuingia barabara kuu ya kutoka Mbeya kwenda Tunduma.

Akizungumza katika hospitali  teule ya Wilaya ya Mbeya muuguzi mkuu wa hospitali hiyo  Sikitu Mbilinyi alisema kuwa katika hospitali hiyo wamepokea  maiti 10 wakiwemo wanawake wanne,wanaume  nne na watoto wawili.

Alisema kuwa katika majeruhi nane,watano ni  wanaume na watutu ni wanawake na kwamba madaktari baada ya kubaini hali za majeruhi hao kuwa mbaya walishauri wapelekwe katika hospitali ya rufaa Mbeya ambapo tayari majeruhi watatu akiwemo mwanamke mmoa wamehamishiwa katika hospitali hiyo.

Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo  ambao  wametambuliwa na ndugu zao kuwa ni pamoja na Mariam Mashambwe na mtoto wake Hamis Chaula,Rebeca Keneth,Petro mgogo,Haruna Jamison na Martin Mwasolikoto.
Mbilinyi aliwataja waliojeruhiwa na ambao wamelazwa  hospiotalini hapo kuwa ni  pamoja na  Kondakta  wa Hiace,Justin Chaula(28)mkazi wa mabatini,Kondakta wa roli Joseph Stephano (22)  mkazi wa mbalizi , aliyekuwa abiria wa roli Ziona Goa  (20),Newton Patrick na dereva wa roli  Amoni Mwakoko.
Akizungumzia jail hiyo majeruhi Ziona Goa alisema kuwa Hiace waliyokuwa wamepanda ilikuwa inatatizo la Breki ambayo ilisababisha gari hilo kuwa na mwendo kasi  huku mbele kukiwa na roli ambalo tayari limeshaingia barabarani.

“Dereva wa gari letu alisikika akisema kuwa breki hazifanyi kazi huku gari yetu ikiwa na mwendo kasi na ghafla tunaona tayari mbele yetu kuna roli limeingia barabarani na ndipo tulipoligonga ubavuni mwa roli hilo”alisema 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amethimitisha kutokea kwa ajli hiyo na kwamba uchunguzi wa ajali hiyo unafanyika ili kuweza kubaini  chanzo cha ajali  hiyo.



  

0 comments: