Pages

Thursday, August 13, 2015

UENDESHAJI USIOZINGATIA USALAMA BARABARANI HUSABABISHA AJALI

Gari yenye namba za  usajili T 828 ACA lilipoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye mtaro, dereva wa gari hilo ambaye alionekana akiwa mbwiiii alikuwa akiliendesha gari hilo kwa kasi na kushindwa kulimudu na hatimaye kutumbukia kwenye mfereji.

Muda mchache baada ya kutokea ajali watu walianza kukusanyika
Dereva wa gari hilo akiwa amezongwa na wananchi na askari waliosogea eneo la tukio



Baadhi ya wanausalama wa eneo hilo walifika kwenye tukio na kushuhudia ajali hiyo

Baadhi ya wakazi na wapita njia walishuhudia ajali hiyo, mmoja wa wpita njia Fredy Njeje alisema aliliona gari akiwa ndani ya gari lake likiwa kwenye mwendo kasi na baadaye ghafla akaona dereva akielekea upande wa kushoto na kutumbukia mferejini.




Baadhi ya wasamaria wakisaidia kuliondoa gari baada ya dereva  kwenye mtereji baada ya dereva kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali ambayo hata hivyo hakuna aliyeumia.

Uendeshaji usiozingatia sheria za usalama barabarani siku zote husababisha ajali na hata kusababisha vifo dereva wa gari hili ambaye inadaiwa alikuwa, ndwiiii kwa ulevi alijikuta akipoteza mwelekeo na kuingia kwenye mfereji usiku huu maeneo ya Soweto karibu na Chuyo cha Kompyuta maarufu kwa jina la Shukurani Center

0 comments: