Pages

Tuesday, October 21, 2014

WAKULIMA WA ZAO LA MPUNGA KATIKA WILAYA YA KYELA,MOMBA NA MBARALI WAPATA MKOMBOZI


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza na wakulima na Wadau wa zao la Mpunga katika uzinduzi wa shirikisho la MTAYArF lillioundwa na makampuni matatu ya Mtenda Kyela Rice Supply,Tanseed International Ltd na YARA Tanzania Ltd katika ukumbi wa Mtenda jijini Mbeya.


 Timu nzima ya shirikisho la MTAYArF wa kwanza ni mkurugenzi wa  kampuni ya Mbegu ya Tanseed  Mashauri,wa pili ni Mwenyekiti wa Bodi wa shirikisho hilo Stella Mutagwaba,Mkurugenzi wa Mtenda Kyela Rice Supply company Ltd George Mtenda na mwakilishi wa kampuni ya M,bolea ya YARA Tanzania
 Mchele ukiwa tayari kwenye vifungashio tayari kwenda sokoni unaoandaliwa na kampuni ya Mtenda Kyela Rice Company Ltd
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtenda Kyela Rice Company Ltd George Mtenda akizungumza katika uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya mbegu ya Tanseed,Mashauri
 Baadhi ya Wakulima na wadau wa zao la mpunga wakiwa katika uzinduzi wa shirikisho hilo katika ukumbi wa mtenda jijini Mbeya
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiwa katika picha pamoja na wadau na wakulima wa zao la mpunga kutoka Wilaya Tatu za Kyela,Mbarali na Momba Mkoani Mbeya
 Mwenyekiti wa Bodi ya MTAYArF  Stella Mutagwaba akitoa taarifa ya shirikisho hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akibadilishana mawazo na wenyeji wake
 Baadhi ya wadau na wakulima wakifuatilia uzindiuzi wa shirikisho hilo


Mwakilishi wa Wakulima wa zao la mpunga katika Wilaya tatu za Momba,Mbarali na Kyela Oden Simkwai akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake.



MKUU  wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  ameyataka makampuni yanayojishughulisha na masuala ya  kilimo ,yasijitengenezee faida kubwa kwa mgongo wa wakulima kwa kuweka mikataba ambayo itamuumizi na kumyonya Mkulima.

Kandoro alitoa  kauli hiyo jana katika uzinduzi wa shirikisho la makampuni matatu   ya Mtenda Kyela Rice Supply Company Ltd,Tanseed International Ltd na Kampuni ya Mbolea ya YARA  Tanzania Ltd ambayo yameungana kwa lengo la kumpunguzia gharama za uzalishaji na kumtengenezea faida mkulima wa zao la Mpunga.

Alisema kuwa kumekuwepo na makamapuni mengi yanayofanya shughuli za kilimo katika mazao mbali mbali lakini yamekuwa yakitengenezea faida kubwa kwa mgongo wa  wakulima  na kumuacha mkulima kuendelea kuwa masikini.

“Ili kilimo kweli kiwe na manufaa kwa mkulima ni lazima mikataba yenu na wakulima iwe mizuri  ambayo itamasidia na kumlinda mkulima  ili anaye aweze kupata faida katika zao analozalisha na kuondokana na umasikini”alisema 

Awali akitoa taarifa ya  shirikisho hilo linaloitwa  MTAYArF  Mwenyekiti wa bodi Stella Mutagwaba  alisema kuwa linatarajia kuwafikia wakulima 6000 wa zao la mpuga katika Wilaya ya Kyela,Mbarali na Momba  ambapo  washirika watafanya kazi kwa pamoja katika myororo wa thamani wa zao la Mpunga.

Alisema kuwa pia shirikisho hilo litakuwa na jukumu la kukabiliana na changamoto za masoko,uzalishaji mdogo na ubora usioridhisha wa zao la mpunga ambapo kila mshirika atakuwa na jukumu maalum la kulingana na uzoefu wake kwenye mnyororo wa thamani  katika zao la mpunga.

Mutagabwa alisema kuwa kamapuni ya Mtenda Kyela Rice Supply itakuwa na majukumu ya kuingia mkataba na wakulima wa  mpunga na kununua , kukoboa  na kuuza mchele  na Tanseed International  itakuwa na jukumu la kuzalisha na kusambaza mbegu bora kwa wakulima kwa bei nafuu huku YARA Tanzania  ikiwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu matumizi bora ya Mbolea kwa wakati sahihi na kiwango sahihi.

 Kwa upande wake mwakilishi wa  wakulima  wa zao la mpunga katika wilaya  hizo tatu, Oden Simkwai alisema kuwa  wanakabaliwa na changamoto mbali mbali ikiwa  ni pamoja na ukosefu wa elimu ya kilimo bora , kukosa soko la uhakika,ubovu wa miundombinu ya barabara na uchakachuaji wa pembejeo za kilimo. 

Simkwai alisema kuwa kutokana na  kuwepo kwa changamoto hizo wakulima wa zao la Mpunga  wataendelea kutumia nguvu nyingi na gharama kubwa katika uzalishaji wa zao hilo bila ya  kupata  faida yoyote na kuendelea kuwa masikini.

 

0 comments: