Pages

Saturday, November 1, 2014

DR MWAKYEMBE ACHANGIA MIFUKO 950 YA SARUJI,UJENZI WA MAABARA KYELA

 Kontena likiwa limejaa mifuko 950 ya Saruji yenye thamani ya Sh 18milioni iliyotolewa na mbunge wa jimbo la Kyela Dk Harrison Mwakyembe kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Wilayani Kyela
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga akipokea mifuko ya saruji 950 yenye thamani ya Shilingi milioni 18 kutoka kwa mwakirishi wa mbunge wa jimbo la Kyela Dr Harrison Mwakyembe,Richard Kilumbo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa maabara katika shule za Sekonsari za Wilaya Kyela ambapo kila shule itakabidhiwa mifuko 50


 Mwakilishi  wa mbunge akitoa taarifa ya mchango huo kutoka kwa mbunge na kusema kuwa ni kuunga juhudi zinazofanywa na wananchi wa wilaya hiyo katika kuchangia maendeleo

KYELA .Mbunge wa jimbo la Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ametoa mifuko ya Saruji 950 yenye thamani ya Sh18milioni kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari  Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo mwakilishi wa mbunge  Mwakyembe,Richard Kilumbo alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi wa Kyela katika kujenga maabara katika shule za Sekondari.

“Rais Kikwete alitoa agizo kwa kila shule  ya sekondari kuwa na maabara ambapo asilimia kubwa ya ujenzi wake unafanywa kwa nguvu za wananchi hivyo mbunge ameona kuna umhimu wa kuungana mkono jitihada zinazofanywa na wananchi wake kwa kuchangia saruji hiyo ili kuasidia kukamilisha ujenzi huu”alisema 

Aidha  Kilumbo amewataka wananchi wa  Kyela wanaoishi ndani na nje ya Wilaya hiyo kuacha siasa za makundi na badala yake kushiriki kwa pamoja katika shughuli za maendeleo ili kufanikisha zoezi hilo ambalo ni agizo la Rais.

“Tunapokuwa katika shughuli za maendeleo siasa tuziweke pembeni na  tuungane  kwa pamoja wanakyela wote  katika shughuli za maendeleo na uhakikisha Wilaya yetu inasonga mbele katika maendeleo,Kyela kwanza Siasa baadae”alisema 

Akizungumza mara baada ya kupokea Saruji hiyo mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Malenga aliipongeza hatua hiyo ya Mbunge Mwakyembe kujitolea saruji ambapo alisema kuwa itasaidia kukamilisha ujenzi wa maabara  katika shule 19 ambapo kila shule itapata mifuko 50 ya saruji.

Alisema kuwa  wananchi wameonyesha juhudi za ambapo hadi sasa wamefikia asilimia 80 bila  ya halmashauri kuchangia chochote  kwani  ilikuwa na bajeti ya ujenzi wa maabara mbili pekee hivyo nguvu kubwa imetumika ni ya wananchi wa Kyela.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya  Kyela alisema kuwa  kyela ina jumla ya shule  za sekondari 22 ambapo tatu  ujenzi wake umekamilika na 19 ujenzi wake wamefikia silimia 80 uliofanywa nguvu za wananchi.

Alisema kuwa  ujenzi huo waa maabara  hizo gharama yake ni  Sh250milioni  ambapo wananchi wamechangia Sh100milioni,halmashauri Sh50milioni na wadau watachangia Sh50milioni.

0 comments: