Pages

Saturday, November 1, 2014

WANANCHI MBOZI WAFUNGA BARABARA KWA MASAA MATATU

 Wananchi  wa kijiji cha Luhanda Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya wakiwa wamefunga barabara kwa mawe na magogo mara baada mwenzao kugongwa na roli na kufa papo hapo na kusababisha abiria na magari kutoka ndani na nje ya nchi kukwama kwa muda wa masaa matatu huku mwili wa marehemu ukiwa pembeni ya barabara hiyo.



Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho akiondoa magogo kwa ajili ya kupisha gari la wagonjwa  mahututi  likiwa limebeba mgonjwa kutoka Mbozi na kupelekwa hospoitali ya rufaa Mbeya,lakini baada ya kupita gari hilo magogo yalirudishwa tena barabarani.

 
Mbozi.Wananchi wa kijiji cha luanda Wilaya ya Mbozi jana walifunga barabara  kuu ya Mbeya Tunduma kwa saaa matatu, kwa kupanga mawe na magogo mara baada ya mwenzao kugongwa na  gari na kufa papo hapo.

Kutokana na tukio hilo la kuziba barabara kuanzia saa 10:00 hadi saa 12:45 jioni  kulisababidha kuwepo kwa foreni kubwa ya magari na kuleta adha  na kero kwa wasafiri na magari yanayotoka na kuingia ndani ya nchi.

Barabara hiyo hutumiwa na nchi za  Zambia,Kongo,Zimbabwe Botswana na  Afrka Kusini kupitia mpaka wa Tunduma  Wilayani  Momba ambapo kuna magari ya aina mbali ikiwa ni pamoja na maroli ambayo yalikuwa yamekwama katika eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika eneo hilo la tukio baadhi ya wananchi hao walisema kuwa matukio ya ajali ya watu kugongwa yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika eneo hilo kutokana na magari kuwa na na mwendo kasi.

“Hivi juzi Oktoba 28 mwaka huu aligongwa mama yetu hapa na alifariki dunia papo hapo lakini alipita mkuu wa wilaya ya Mbozi  Michael Kadege na kutuahidi kuwa baada ya siku tatu yatajengwa matuta katika eneo hili lakini hakuna kilich ofanyika na leo amegongwa mtu mwingine hili halikubaliki”alisema mkazi mmoja wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina Elias Simbeye

Simbeye alisema kuwa wameamua kuziba barabara ili kuikumbusha serikali kuwa matuta yanayatakiwa haraka katika eneo hilo ili kuweza kuokoa maisha ya watu kutokana na kugongwa na magari mara kwa mara katika eneo hilo.

Alisema kuwa eneo hilo lina miteremko mkari kwa pande zote mbili lakini magari yamekuwa yakitumia mwendo kasi bila ya tahadhari kutokana na kijiji hicho kuwa na watu wengi ambao wamekua wakivuka ng`ambo ya pili kwa ajili yakufuata mahitaji Sokoni.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Luanda Blaya Msongole alisema kuwa wananchi wamepatwa na hasira kutokana na ahadi aliyokuwa ameitoa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi hivi karibuni ilipotokea ajali ambapo pia walitaka kufanya tukio kama hili.
“Mkuu wa Wilaya alipita hapa na kuwaomba wananchi watulie huku serikali Wilaya ikifanya jitihada za kuhakikisha matuta yanawekwa hapa baada ya siku tatu kitendo ambacho hakijafanyika hivyo ili ndilo linatupa shida hapa”alisema 

Jeshi la polisi Mkoa wa Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo  askari wake walifungua barabara hiyo  bila kutumia nguvu na kufanikiwa magari hayo kuanza kupita majira ya saa 12:45 jioni.

0 comments: