Pages

Saturday, November 1, 2014

MADIWANI MOMBA NUSURA WARUSHIANE MAKONDE NDANI YA KIKAO CHA BARAZA

 Diwani wa kata ya Chiwezi (CCM) Emmanuel Punte  Wilaya ya Momba  Mkoani Mbeya aliyenyosha mkono akirushiana maneno na Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka  na kusababisha kutaka kurushiana ngumi katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo.

  Diwani   wa kata ya  Mkulwe  wa (CCM) ,Mathew Chikoti akimsihi Diwani wa kata ya Chiwezi (CCM) Emmanuel Punte kuacha malumbano ndani ya kikao cha baraza la madiwani


Momba:Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Momba jana nusurawarushiane  makonde ndani ya kikao cha baraza la madiwani  baada yakutokea  malumbano makali ya kutaka kuvunjwa kamati mbali mbali  nakuteua  wajumbe wapya.
Vurugu hizo zilianza mara baada ya  kutolewa hoja na Diwani   wa kataya  Mkulwe  wa CCM ,Mathew Chikoti  ya kuwa   utaratibu uliotumikakatika kuteua wajumbe hao  haukufuata kanuni   za baraza hilo kutokanana maelekezo ya serikali.

“Kutokana na  elimu tuliyopewa na maboresho ya kuzijua kanuni mbalimbali yaliyofanyika hivi karibuni tumebaini kuwa ni mambo mengi ambayo meza mmekuwa mkituficha hivyo hata utaratibu uliotumika katika kuteua wajumbe wa kamati haukuwa sahihi kwani haukufuata kanuni za barazaletu”alisema  diwani  Chikoti

Hoja hiyo ilipingwa na Mwenyekiti wa halmashauri Bernad Sicholongwealiyekuwa akiongoza  kikao hicho hali iliyosababisha kutokea kwa mvutano mkali na kufikia madiwani kurushiana lugha chafu  ndani ya kikao hicho

Hali iliendelea kuwa mbaya mara baada ya Diwani wa kata ya
Tunduma(CHADEMA) Frank Mwakajoka ambaye aliomba mwongozo kutoka kwa mwenyekiti ambapo  hoja hiyo ilipingwa vikali na diwani  wa kata yaChiwezi(CCM)  Emmnuel  Punte ambapo alisema kuwa diwani huyo hanauwezo wa kutoa mwongozo huo hivyo na Mwenyekiti hawezi kumsikiliza.

Diwani huyo wa Chiwezi alimtaka Mwenyekiti kutovunja kamati hizo nakuendelea na baraza”kwani mimi tangu nimechaguliwa sijawahi kuingiakatika kamati ya fedha hivyo tuacheni tuendelee kuwepo katika kamatihii”alisema

Baada ya kauli hiyo ndipo madiwani hao wakaanza kurushiana maneno  na hata kufikia kutaka kurushiana makonde  hadi hapo mwenyekiti alipoamua kumtoa nje diwani   huyo wa  kata ya Chiwezi

Pamoja  na kumtoa diwani huyo nje bado hali iliendelea kuwa si shwari ndani ya baraza hilo ambapo madiwani wengine wa  CCM  waliendelea kumtuhumu mwenyekiti wao kuendesha kikao hicho kibabe ambapowaliendelea kumsisitiza kuwa aendeshe kikao hicho kwa kufuata kanuni.

“Mwenyerkiti unachokifanya hapa ni kutuburuza hatuwezi kuendelea nakikao hicho hadi hapo utakapotoa majibu ya kuvunja kwa kamatitunaomba  utusomee kanuni  na uendeshe kikao kwa kufuata kanunihizo”alisema diwani wa Nkangamo (CCM)Winston  Simwelu

Hali  hiyo ilianza kuwa tulivu mara baada ya afisa utumishi wa
halmashauri ya wilaya  hiyo Ameliye Mfugale  kusoma kanuni  kuwa kama wajumbe watakuwa hawajaridhika na uteuzi wa wajumbe wakamati halmashauri ianweza kuvunja  kamati hizo na kufanya uteuzi upya wakati wowote endapo kama wasioridhika watafikia theruthi mbili.

Baada  ya afisa utumishi  huyo   kueleza kanuni hiyo  ndipo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo Anton Mwantona aliposimama  na kueleza kuwa  ataitisha kikao maalumu kwa ajili ya kuvunja kamati hizo  na  kuteua wajumbe wapya endapo kama theluthi mbili za wajumbe zitafikiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Momba Abihudi Saidea alisema kuwaanashangazwa na hatua ya madiwani kulumbana katika kikao cha baraza lamadiwani na kuwataka kuimarisha ushirikiano katika kuleta maendeleo.

Alisema kuwa kikao hicho kinapaswa kuendeshwa kwa kufuata kanuni nasheria za baraza la madiwani ili kuondoa migongano mbayo inawezakutokea wakati kikao hicho kinaendelea.


0 comments: