Pages

Thursday, November 6, 2014

MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU (GEFP)WAFUNGUA OFISI ZA KANDA MBEYA

 MENEJA wa masoko wa GEFAloyce Ntukamanzina , akiwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa ofisi za kanda ya nyanda za kuu kusini ziliopo Delha House Lupaway Uhindini  jijini Mbeya


 Meneja wa GEFP  Mkoa wa Mbeya Ramadhan Sossora akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
 Mwandishi wa habari  wa Bomba FM na mratibu wa hafla  hiyo akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mfuko GEFP
 Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo
 Meneja Masoko wa GEFP,Aloyce Ntukamanzina akitoa taarifa ya uetekeleza  katika hafla hiyo
Meneja Masoko Aloyce Ntukamanzina akisikiliza kwa makini maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo



MBEYA .Mfuko wa mafao ya kustaafu (GEPF) umefanikiwa kukusanya Sh37.29bilioni kutoka kwa wanawachama wake 76,000 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 2004 hadi Juni 2014.

Hayo  yalisemwa  jana na meneja masoko wa GEP, Aloyce Ntukamanzina katika  uzinduzi wa ofisi ya tisa ya nyanda za juu kusini katika  eneo la uhindini jijini Mbeya.

 Ntukamanzina alisema kuwa mfuko huo umekuwa ukifanikiwa mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2004 ilikuwa na wanachama 16,131 na kufanikiwa kukusanya Sh5.1bilioni.

Alisema kuwa katika kipindi hicho cha miaka 10  mfuko huo pia umeweza kulipa mafao kwa wanachama wake 76,000  zaidi ya Sh12.73bilioni  wakati  mwaka 2004 walilipa mafao  Sh67.1milioni kwa wanachama 16,131.

Aidha alisema kuwa  mfuko huo pia umeweza kupata mafanikio makubwa katika  mpango wa hiari wa kujiwekea akiba  katika kipindi cha miaka mine tangu ulipoanzishwa mwaka 2010.

Alisema kuwa  katika kipindi hicho wameweza kukusanya zaidi ya Sh5bilioni kwa wanachama 35,481 waliosajiliwa na kwamba mpango huo unawahusu wanachama walioajiriwa,wasioajiliwa  na wafanyabishara.

Meneja huo alisema kuwa sababu kubwa ya kuanzisha mpango huo maalum ni kuwawezesha watanzania wengi kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kwani uwiano wa mifuko ya pensheni iliyopo nchini idadi ya wanachama wanaohudumiwa na mifuko hiyo haiendani.

“Tanzania tuna watu zaidi ya 48milioni na tunamifuko ya sita lakini wanaopata huduma katika mifuko hii ni watanzania 1.8milioni pekee,kwa hiyo tunaona  jinsi kunachangamoto kubwa kwa mifuko hii ya pensheni kuwafikia watanzania walio wengi”alisema





0 comments: