Pages

Wednesday, November 26, 2014

KAMPUNI YA UNUNUZI WA KAHAWA MBEYA YA CMS YATOA MSAADA WA MIFUKO YA SARUJI RUNGWE


 Mkurugenzi  Mkuu wa kampuni  ya kununua kahawa Mkoani Mbeya (CMS)Yogesh Modhwadia akiwa na Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya

 Mwakilishi wa kampuni ya kunuanua kahawa Mkoani Mbeya CMS Ephrahimu Kasanga akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari Wilayani humo.


 Mkurugenzi  Mkuu wa kampuni  ya kununua kahawa Mkoani Mbeya (CMS)Yogesh Modhwadia akielezea kazi zinazofanywa na kampuni yake katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe wakati kampuni hiyo ikikabidhi msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara

 Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crisipin Meela akifurahia jambo baada ya kupokea taarifa ya Kampuni ya CMS ya kukabidhiwa mifuko 60 ya Saruji


Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mwenye shati  nyeupe akiwa ameshikana mkono na mwakilishi wa kampuni ya CMS baada ya kukabidhiwa mifuko 60 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari




RUNGWE.Wananchi Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wametakiwa kuwapuuza wanasiasa ambao wanawashinikiza kugoma  kuchangia  ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari  ili kuepuka watoto wao kufanya vibaya katika masomo ya sayansi.


Kauli hiyo imetolewa  jana na mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela alipokuwa akipokea mifuko 60 ya Saruji yenye thamani ya Sh1.2milioni kutoka kwa Kampuni ya ununuzi wa kahawa  mkoani Mbeya (CMS )ikiwa ni mchango wa ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari Wilayani humo.


Meela alisema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipita kwa wananchi na kuwashinikiza wagome kuchangia ujenzi wa maabara na kusababisha baadhi ya maeneo utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa kila shule kusuasua.


“Katika suala  hili la ujenzi wa maabara siyo ni la Serikali pekee bali linahitaji nguvu za wananchi  hivyo wananchi wanatakiwa kuwapuuza hawa wanasiasa wetu ili kuweza kukamilisha agizo la Rais,hivyo sioni sababu ya wanasiasa kutaka kutuharibia utaratibu tuliojiwekea na wananchi katika ujenzi wa maabara zetu”alisema 


 Meela alisema kuwa  kuhusu ujenzi wa maabara umefikia asilimia 90  na kwamba wilaya hiyo ina jumla ya shule za sekondari 43 na halmashauri ya Rungwe imechangia Sh.90milioni na Busokelo imechangia Sh101milioni katika ujenzi huo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa samani.


Akizungumza wakati wa kukabidhi  Saruji hiyo mwakilishi wa kampuni ya CMS Ephraim Mwakabaja alisema kuwa mbali ya  kampuni hiyo kununua kahawa kwa wakulima wa Wilaya ya Ileje,Mbeya vijijini,Mbozi na Rungwe  pia inajihusisha katika kuchangia maendeleo ya wananchi katika maeneo hayo.


Alisema kuwa  kama kampuni  wanafahamu umuhimu wa maabara katika shule za Sekondari hivyo wameamua kuchangia saruji hiyo ili  kuwasaidia watoto wa wakulima wa kahawa kufanya vizuri katika masomo ya Sayansi.


Aidha alisema kuwa  mbali ya mchango huo wa Saruji kwa Wilaya ,kampuni hiyo imeweza kuchangia ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Bujinga kwa kutoa  fedha tasilimi Sh200,000 .








0 comments: