Pages

Thursday, January 16, 2014

Ajali yaua watu wawili na kujeruhi 23 Mbeya



 Wakazi wa mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya wakiangalia gari aina ya Coaster mara baada ya kogongana na roli eneo la Mlima Mbalizi Wilaya ya Mbeya.



WATU wawili wakufa  papo hapo  jana  na wengine 23 kujeruhiwa, baada ya basi aina ya Coaster waliyokuwa wakisafiria kutoka Jijini Mbeya kuelekea Tunduma kugongwa kwa nyuma na Lori la mizigo katika eneo la mlima Mbalizi Wilaya ya Mbeya vijijjin.


Aidha katika  katika hali isiyokuwa ya kawaida askari wa kutuliza ghasia waliofika muda mfupi baada ya kutokea ajali hiyo walilazimika kufyatua lisasi hewani ili kuwatawanya watu walionza kupora vitu baada ya Lori hilo kuanguka  lilimwaga bidhaa mbalimbali za madukani, zikiwemo sabuni hali iliyofanya wananchi kuanza kuvamia kwa lengo la kupora.

Akizumgumzia  ajali hiyo mmoja wa shuhuda  John Mwakambo  alisema kuwa  ilitokea jana majira ya saa 10:45, wakati magari hayo yakitelemka katika mtelemko mkali wa mlima Iwambi ,karibu na mji mdogo wa Mbalizi.

“ Lori hilo la mizigo lenye namba za T 101 CLR na Tela lake T 859 BZW aina ya Scania liliigonga Coaster hiyo yenye namba T 910 BFB kwa nyuma kwani lilionyesha kama kulikuwepo na tatizo la kuharibika mfumo wa breki”alisema

Akifafanua zaidi shuhuda huyo, alisema wakati Lori hilo likishuka kwa kasi mbele kulikuwa na gari nyingine aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 370 AST lililokuwa likipandisha hivyo kumchanganya dereva wa Lori hilo hivyo kuligonga kwa nyuma basi hilo la abiria.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki alithibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kusema watu wawili walifia papo hapo ambao hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika mara moja.


Alisema kuwa  kuwa kati ya majeruhi hao 23, majeruhi 17 walipelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na wengine sita walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi iliyoko wilaya ya Mbeya Vijijini

0 comments: