Pages

Monday, January 13, 2014

Amuua kaka yake kwa kulipiza kisasi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwanadmizi wa polisi Ahmed Msangi.


Watu wawili wameuawa katika matukio tofauti  Mkoani  Mbeya akiwemo mkazi wa kijiji cha Kapele  Wilaya ya Momba aliuawa kwa kuchomwa kisu mgongoni na mdogo wake kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya kutangaza mtuhumiwa kuwa alitorosha mke wa mtu.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi  Ahmed  Msangi amewataja waliouawa kuwa ni pamoja na Adam Silumbe (27)  mkazi wa kijiji cha Kapele Wilaya  ya Momba na Bicco Mwakabibi (28) mkazi wa kijiji cha Lema Wilaya yha Kyela.

Akizungumzia  matukio hayo  Msangi alisema kuwa  tukio la mauaji ya Adam Silumbe lilitokea  Junuari 10mwaka huu majira ya saa 3:000 usiku  baada ya marehemu kuchomwa kisu mgongoni na mdogo wake Bonny Silumbe  katika kijiji cha Kapele Wilaya ya  Momba.

Alisema kuwa baada ya kufanyika kwa tukio hilo marehemu alikimbizwa katika hospitali ya serikali  Wilaya ya Mbozi ambapo alifariki jana majira ya Saa 3:30 asubuhi  alipokuwa akiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Msangi alisema kuwa chanzo cha tukio hilo na mtuhumiwa alitoroka mara baada ya kufanya tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa kwa  familia yake kwa ajili ya mazishi.

Katika tukio lingine marehemu Bicco Mwakibibi aliuawa  kwa kupigwa sehemu mbali mbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia  sheria mkononi  wakitumia silaha za jadi  mawe na fimbo kwa tuhuma za wizi kayika kijiji cha  Lema Wilaya ya Kyela.

Kamanda Msangi alisema kuwa  marehemu na mwenzake wanatuhumiwa kuvunja kibanda cha biashara na kuiba na kwamba baada ya tukio wenzake  alikimbia na kwamba juhudi za kumtafuta zinafanyika.

0 comments: