Pages

Monday, January 13, 2014

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHFI) watoa msaada wa vifaa tiba

Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii DK Seif Rashid akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Tiba kwa Mikoa ya Tanga na Mbeya katika ukumbi  Hospitali ya Mkoa wa Mbeya   



Naibu Waziri wa  afya na ustawi wa jamii   Dk Seif Rashid jana amekabidhi vifaa tiba kwa mikoa ya Tanga na Mbeya  vyenye  thamani  ya Sh989.1 milioni kwa ajili ya mradi wa mama na motto unaotekelezwa  kwa ushirikiano   na mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHFI) na benki ya maendeleo ya watu wa Ujerumani(KfW).


Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo naibu Waziri huyo alisema kuwa serikali inatambua umuhimu na kuenzi jitihada zinazolernga kuboresha afya ya mama na mtoto kwani hakuna haja ya mama mjazito kupoteza maisha  wakati wa kuleta kiumbe hai.

“Kutolewa kwa vifaa hivyo ni ishara ya kuwa tunaweza kuboresha huduma za akina mama wajawazito na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ikiwa tutashirikiana kukusanya nguvu za pamoja na kuliona suala hili kuwa ni wajibu wa kila mmoja”alisema 

Alisema kuwa  kupunguza idadi ya vifo vya wakina mama wajawazito inawezekana kwani  takwimu zinaonyesha kuwa nchi ya Uingireza kuna vifo sita kati ya wakina mama wajawazito 100,000 kwa mwaka na wa  Tanzania  ni vifo 454  kati ya wakinamama 100,000 huku mikoa ya Iringa na Mbeya ikiwa na vifo chini ya 200 kati ya wakina mama 100,000 kwa kila mwaka.

Aidha ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa Tanga na Mbeya kuhakikisha baada ya miezi sita kuanzia sasa ziwe zimewasilisha madai ya fedha za tele kwa tele  na kuzipata fedha hizo ili kuweza kuboresha  huduma ya afya.

Awali akitoa taarifa ya  mradi huo Kaimu Mkurugenzi mkuu  wa NHFI Hamisi Mdee alisema kuwa  katika mradi huo jumla ya walengwa 74,099 wameshafikiwa ambao ni sawa na asilimia 105 kati ya lengo la kuwafikia akina mama wajawazito 70,000 kufikia Desemba 2014.

Alisema kuwa kupitia mradi huo kiasi cha Sh644.1milioni zimelipwa kwa vituo vya matibabu vya mikoa ya Tanga na Mbeya vilivyotoa huduma  kwa akina mama wajawazito na Sh400.4 zimetumika kulipia familia za akina mama hao ili kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (chf)  na hivyo kuziwezesha halmshauri 12 za mikoa ya Mbeya na Tanga kuomba fedha za tewle kwa tele kutoka NHFI.

Mdee alisema kuwa katika utekeleza wa mradi huu kuna changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na vituo vya huduma kutowasilisha madai yao kwa huduma walizotoa kwa akina mama wajawazito pamoja na kuwa wamekuwa wakilipwa na NHFI na wananchi  kutofikiwa na elimu kuhusu huduma za usalam na huduma za mifuko hiyo miwili.


0 comments: