Pages

Monday, January 13, 2014

Uwanja wa soka wa Sokoine wa pili kimapato



Mwenyekiti wa chama cha Mpira  Mkoa wa Mbeya (MREFA)Elias Mwanjala  amesema kuwa uwanja wa kumbukumbu ya sokoine umekuwa ni  uwanja wa pili kimapato ukiongozwa na uwanja wa Taifa kutokana na kuwepo kwa timu ya Mbeya City.


Mwanjala alisema kuwa  kutokana na kuwepo kwa timu ya Mbeya City kumeongeza idadi kubwa ya mashabiki ambao wamekuwa wakiingia katika uwanja huo mara timu hiyo inapokuwa inacheza kuwezesha kuingiza fedha nyingi ambazo hazikuwahi kutokea huko nyuma.

“Katika hili lazima tuseme wazi kuwa uwan ja huu wa Sokoine umekuwa pili kimapato ukiongozwa na  na ule wa Taifa sababu ya kuwepo kwa mbeya City kwani timu hii imekuwa na mashabiki ambao wakuwa wakijaa uwanjani mara timu hii inakuwa na mechi”alisema

Alisema kuwa mashabiki hao wa Mbeya City pia wamekuwa wakijitolea kwenda  kushuhudia mechi za nje za timu yao kama vile jijini Dar mechi ya Simba na Azam na Tanga ambapo pia waliweza kuongeza mapato katika michezo hiyo.

“Awali uwanja wa sokoine ulikuwa ukipata mapato makubwa  wakati wa mechi za Simba na Yanga zinapokuja kucheza hapa lakini hata hivyo ujazaji wa mashabiki hauwezi kuifikia timu ya Mbeya City ilipokutana na timu ya Yanga na nyinginezo katika  mzunguko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom”alisema

Alitoa mfano wa mechi  kati ya timu Yanga  Afrikan na Mbeya City iliyofanyika ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 iliingiza wato 20,000 na mapato yalikuwa ni Sh100 milioni  katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini  hapa.




0 comments: