Pages

Monday, January 13, 2014

Ukarabati wa uwanja wa Sokoine wafikia asilimia 95%



BAADA ya kusuasua  na kuzua hofu kubwa kwa wadau wa soka mkoani Mbeya,Hatimaye kazi ya kupanda nyasi ndani ya uwanja wa Sokoine imekamilika kwa asilimia 95, tayari kwa michezo ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jana , Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya (Mrefa), Elius Mwanjala, zoezi hilo limeghari kiasi cha shilingi milioni 22.3 hadi kukamilika kwake.

Hata hivyo, Mwanjala aliwataka wadau wa soka kujitokeza ili kusaidia kiasi cha shilingi milioni 4 ili ziweze kusaidi kazi iliyobaki ya asilimia tano, kwa kuwa  chama hicho kimeishiwa  na hakina uwezo wa kupata  fedha hizo kwa haraka.

Aidha, amewatoa hofu wadau wa soka na kusema asilimia tano iliyobaki haiwezi kuasili ratiba ya mechi za mzunguko wa kwanza na kwamba michezo yote ya mzunguko wa pili iliyokuwa ichezwe ndani ya uwanja huo itafanyika bila kikwazo chochote.

Alisema kama fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 4 zikipatikana kwa muda muafaka uwanja huo unaweza kukamilika kwa asilimia 100 ndani ya wiki ijayo hivyo kutoa mwanya mechi za mzunguko wa pili kuchezewa ndani ya uwanja huo mkongwe wa Sokoine.

Mwanjala alisema  kuwa pamoja na kufikia hatua hiyo bado kuna changamoto inayowakabili ikiwa  ni pamoja na deni la kiasi cha shilingi  milioni 13.8 lililotokana na wadau kukikopesha   fedha  hizo  chama hicho kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo.

Aidha  aliwashukuru wadau wote waliojitokeza kusaidia kwa hali na mali zoezi zima, lakini shukurani kubwa amezielekeza kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kuamua kuamua kusaidia nguvu kwa kutoa askari wa jershi la kujenga taifa (JKT).

Akifafanua zaidi, Mwanjala alisema kitendo cha JKT kuongeza nguvu kimechangia kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa wakati kwa upandaji nyasi ndani ya uwanja huo.

Uwanja wa Sokoine Mbeya unatumiwa na timu mbili za ligi kuu ya Vodacom, ambazo ni Mbeya City inayofanya vizuri , pamoja na Tanzania Prisons,

0 comments: