Pages

Thursday, January 2, 2014

Mwanamke auawa kwa kupigwa na mume wake




WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoani Mbeya akiwemo mwanamke mmoja Huruma Laiton (20) amerariki dunia  jana akiwa anapatiwaa  matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya baada  ya kupigwa  na mume wake kwa madai  ya kumfumania akifanya mapenzi na binamu yake ndani ya nyumba yao katika kijiji cha  Inyala Iyunga mkoani hapa.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana (juzi)  majira ya saa 10:00 jioni katika kijiji cha Inyala Iyunga Mkoani Mbeya ambapo marehemu anadaiwa kukutwa  na mume wake Ezekiel Mwakabenga (21)akifanya mapenzi na binamu yake.

Alisema kuwa mtuhumiwa Mwakabenga alimpiga marehemu sehemu mbalimbali  za mwili wake kwa kutumia ngumi,fimbo na mateke na baadae kikimbizwa katika hospitali ya rufaa  Mbeya ambapo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda Msangi alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na kwamba anatarajia kufikishjwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika na mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya.

Aidha  Msangi ametoa wito kwa wanandoa kutatua migogoro yao ya kifamilia kwa njia ya kukaa meza moja ya mazungumzo ili kufikia muafaka wa migogoro yao kwa njia ya amani badala kujichukulia sheria mkononi  na kusababisha vifo.

Wakati huo huo mkazi  wa kijiji  cha Itezi mashariki jijini Mbeya  Christopher Myamba (20) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Ndele baada kutokea kwa mzozo baina ya marehemu akiwa na rafiki yake na mtuhumiwa.

Kamanda Msangi alisema kuwa marehemu akiwa na rafiki yake walikutana na njiani na kundi la vijana wanne akiwemo mtuhumiwa wakiwa wamelewa na kuwafanyia fujo na ndipo marehemu alipochomwa kisu shingoni.

0 comments: