Pages

Sunday, August 24, 2014

BARAZA LA UVICCM WILAYA YA CHUNYA LAFANYIKA KWA VIJANA KUTAKIWA KUSIMIAMIA NA KUDHIBITI MAADILI YA WANACHAMA NA VIONGOZI WAO

 Mwanachama na mkereketwa wa CCM  Wilaya ya chunya Joshua Mlambalala  akitoa malalamiko yake kuhusu Taasisi ya kupumbana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Chunya,katika semina fupi iliyofanyika kabla ya kuanza baraza la UVCCM Wilayani humo katika ukumbi wa chama hicho.



 Wanachama na wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Chunya wakisikiliza kwa makini

 Katibu Msaidizi wa CCM  Wilaya ya Liawale Mkpoani Lindi Timoth Mzava akiwa katika picha ya pamoja  na makada wenzake  akiwemo mjumbe wa baraza la UVCCM   Mkoa wa Mbeya akiwakilisha Wilaya ya Ileje Mary Mwanisongole katika mnara wa miaka 50 ya Uhuru Wilayani Chunya
 Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Chunya Saul Mwaisenye akizungumza wakati wa ufunguzi wa baraza la vijana Wilayani humo

 Mjumbe wa baraza kuu ya UVCCM Taifa Neema Mwandabila akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo Wilaya ya Chunya 


Chunya .Vijana na wanachama wa chama cha mapinduzi  Wilaya ya  Mbeya  wametakiwa  kusimamia na kudhibiti maadili ya viongozi na wananchama badala ya kutumika na wanasiasa wanaotaka madaraka kwa lengo la kujinufaisha wao na familia zao.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu msaidizi wa umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi Timoth Msava katika  mkutano wa baraza la vijana la Wilaya ya Chunya lililofanyika jana katika ukumbi wa  chama hicho.

Alisema kuwa kazi ya vijana ni kuhakikisha  wanachama na viongozi wanakuwa na maadili mazuri kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama kwa lengo la kujenga chama na kurudisha imani ya chama kwa jamii nzima.

“Vijana tunapaswa kubadilika na kufanya kazi kwa kufuata kanuni za chama chetu kwani maadili ya  baadhi ya wanachama na viongozi wetu siyo mazuri na badala tumegeuzwa na kuwekwa mifukoni mwa wagombea na kufanywa madaraja ya kupatia madaraka  kwa masilahi yao binafsi”alisema
Akitoa taarifa ya Jumuia hiyo Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Chunya Saul Mwaisenye  alisema kuwa  kuna kero ambazo zisipopatiwa ufumbuzi haraka  vijana wengi ambao ni wakulima na wafugaji watakata tamaa na kuichukia serikali yao

Mwaisenye alizitaja kero hizo kuwa ni pamoja na  vojana kutotengewa maeneo ya kuchimba dhahabu ili kuondoa mzozo unoajitokeza mara kwamar kati yao na wawekezaji na kusababisha kuijengea chuki serikali yao.

Alizitaja kero nyingine kuwa ni pembejeo za kilimo zinazotolewa kama ruzuku na serikali kutofika kwa wakati na asilimia 10  zinazotakiwa kutolewa na halmashauri ya Wilaya kwa ajili kukopeshwa  vikundi vya vijana na akinamama  hazitolewi.

“Na kama zinatolewa basi wahusika huenda wanakopeshana wenyewe au kwa upendeleo kwani taarifa zake hazitolewi na ni moja ya malalamiko ambayo tunayapata kutoka kwa vijana wa Wilaya ya Chunya kuwa hawapati fedha za mikopo hiyo”alisema

0 comments: