Pages

Sunday, August 24, 2014

VIJANA CCM WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI,UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa Neema Mwandabila akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa baraza hilo Wilaya ya Chunya lililofanyika katika ukumbi wa chama hico Wilayani humo


 Mmoja wa viongozi wa kikundi cha ulinzi na usalama cha UVCCM  (GREEN GADI)akitoa ishara ya heshima wakati wa mgeni rasmni alipokuwa akiingia ukumbini
 Baraza hilo lilipata mgeni kutoka nchi ya  CROATIA  aliyejitambulisha kwa jina la Leta aliyekuwa ameongozana na mgeni rasmi mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa Neema Mwandabila

Katibu msaidizi wa UVCCM Wilaya ya Liwale Mkoa wa Lindi Timoth Mzava akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo na kuwataka vijana kusimamia na kudhibiti  maadili ya viongozi na wanachama wake badala ya kubaki kutumika na watu wanaotaka madaraka kwa masilahi yao binafsi na familia zao.

CHUNYA.  Mjumbe wa baraza kuu la Taifa Neema Mwandabila amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika hivi karibuni badala ya kubaki kuwabebea mabango wazee.
 
Akizungumza jana katika  mkutano wa baraza la UVCCM Wilaya ya Chunya  uliofanyika katika ukumbi  wa chama hicho alisema kuwa  ni wakati wa vijana kutumia fursa  zilizopo ikiwa ni pamoja na uchaguzi huo  kwa  kushiriki chaguzi mbali mbali na kugombea na nafasi mbali mbali za uongozi.

“Msimamo wa  chama cheti na kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika chaguzi mbali mbali  huku tukiwa na lengo moja la kushinda  na kushika dola  hivyo kama vijana tunanafasi pia kuhakikisha tunagombea na kushinda badala ya kubaki kuwabebea mabango wazee”alisema 

Aidha Mwandabila  alisema kuwa  ni kazi ya kuhamasisha  jamii kwenda kujiandikisha katika dafatari la wapiga kura mara  utaratibu ukapoanza ili kuweza kuwa na wapiga kura wengi ambao wamejiandikisha na kitambulisho cha mpiga kura.

Alisema kuwa marekebisho ya dafatari hilo yanatarajia kuanza hivi karibu hivyo ni vema vijana wakajiandaa  kwa kuhamsisha familia zao na jamii inayowazunguka kwani kutoka kufanya hivyo  uwepo wa Uvccm utakuwa hauna maana.

Kuhusu Katiba Mpya mjumbe huyo alisema kuwa  vijana wanapaswa kuzingatia msimo wa chama hicho wa kuwepo kwa serikali mbili kwani hakuna  nafasi ya  kuhoji  kuhusiana mfumo huo wa serikali mbili.

“Nilazima  kama vijana tushiriki katika kuhamasisha wananchi kuikubali serikali mbili kwani huo ni msimo wa chama chetu kwa la kuulinda muungano wetu hakuna sababu kwa sisi vijana kuendelea kuhoji  suala hili kwani tayari linaeleweka kwamba ni lazima katiba yetu ielekeze uwepo wa serikali mbili”alisema 

Mwandabila alisema kuwa  kuna muda utafika kwa katiba hiyo kwenda kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya ndiyo au hapana hivyo ni wajibu wa vijana kushiriki kikamilifu katika  kufanya kampeni  ya kuhakikisha wananchi wanaikubali kwa kuwa na serikali mbili.

0 comments: