Pages

Monday, August 4, 2014

COCACOLA KWANZA YATOA BURUDANI KABAMBE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE


 Mcheza show wa kikundi cha muziki  cha jijini Mbeya akitoa burudani katika banda la Cocacola katika maonyesho ya Nane nane kanda ya nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


 Vinywaji baridi vinavyozalishwa na kampuni ya cocacola kwanza Mbeya vikiwa tayari katika maonyesho ya nanenane Mkoani Mbeya

 Wafanyakazi wa kampuni ya vinywaji baridi CocaCola wakiwa katika picha ya pamoja
 Mamia ya watu waliojitokeza katika banda la CocaCola kushuhudia burudani ya muziki iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maonyesho ya nane nane


 Mamia ya watu wakiangalia kwa makini jukwaani burudani inayotolewa na kikundi cha wacheza Show katika banda la CocaCola katika maonyesho ya nanenane



Kampuni ya vinywaji baridi ya CocaCola Kwanza imeandaa burudani ya muziki kwa wateja wake katika maonyesho ya nane nane kanda ya nyanda za juu kusini  yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika viwanja vya John Mwakangale jiji Mbeya .

Akizumgumza na mtandao huu ofisa mauzo  na masoko kanda nyanda za juu kusini Rashid Mgonja alisema kuwa kampuni hiyo kama kampuni zingine imejitosa katika maonyesho hayo kwa lengo la kushiriki pamoja na wakulima na wateja wao katika kusherehekea sikukuu hiyo ya nanenae.

Alisema kuwa maonyesho hayo ni muhimu kwa kampuni hiyo kutokana na kuwa vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo vinapendwa na kutumiwa na wananchi hivyo ni vema kampuni hiyo ikatoa burudani nzuri ya muziki kwa ajili ya kuwaburudisha wateja wao.

Aidha amewataka wananchi wote wakatembelea katika banda hilo kwa ajili ya kujipatia vinjwaji baridi ikiwa ni pamoja na burudani ya muziki ambayo inaendana na maonyesho hayo ya nanenane na kupata sehemu nzuri ya kupumzika huku akipata kinywaji na burudani

0 comments: