Pages

Thursday, August 7, 2014

JESHI LA POLISI LAWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA KWA MABOMU YA MACHOZI

 Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Mwambigija akizungumza na mkuu wa polisi Wilaya  ya Mbeya (OCD) Richard Mchomvu mara baada ya kuzuiliwa kubeba maiti mkononi ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Ezekiel King aliyefariki dunia juzi mara baada ya kuugua ghafla  gerezani wakati  akitumikia kifungo cha miaka saba



 Askari polisi wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa Mbeya wakiwazia Chadema kubeba mwili wa marehemu huyo mkononi





Jeshi la polisi Mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwazuia wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na waombolezaji  kuubeba  mikononi mwili wa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Itiji  Ezekiel  King kwa tiketi ya chama hicho kwa lengo la kutembea nao kwa miguu kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya hadi nyumbani kwake Itiji.


Baada ya mabomu hayo kurushwa viongozi na wafuasi wa chama hicho walilazimika kulibwaga chini jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu na kulitelekeza na kuanza kukimbia.


Marehemu alifariki juzi katika hospitali ya rufaa Mbeya alikopelekwa  kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua ghafla katika gereza la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo cha miaka Saba baada ya kupatikana na kosa la kuzuru mwili .


Hatua  ya jeshi la polisi kuamua kuchukua uwamuzi huo ni baada ya viongozi na wafuasi wa Chadema kuuchukua mwili wa marehemu kutoka chumba cha kuhifadha maiti katika hospitali ya rufaa  huku mwili ukiwa kwenye toroli maalum la kubebea wagonjwa  na walipofika katika geti hilo ndipo walipoubeba mkononi.


Baada ya wafuasi hao kuubeba mwili huo mkononi ndipo mkuu wa polisi Wilaya ya Mbeya (OCD)alipowazuia na kuwataka kutumia  gari kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kufanya maandamano.


Hali hiyo ya mabishano ilisababisha kutokea kwa taharuki kubwa ambapo ghafla gari mbili zilizokuwa zimewabeba askari  kanzu na askari wa kutuliza ghasia huku zikipeperusha bendera nyekundu zilipofika katika eneo la mnara wa kumbukumbu ya mashujaa na kuwazuia kwa mbele na kuanza kurusha mabomu ya machozi na kusababisha wafuasia hao kulibwaga chini jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu na kuanza kukimbia.


Askari polisi waliokuwepo katika eneo hilo waliamua kulibeba jeneza hilo na kulirudisha katika chumba cha kuhifadhia maiti na ndipo Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu)alipowatuliza wafuasi hao kwa kuwataka watulie kwani wanaenda  kwenye kikao cha pamoja na  OCD kurishughulikia suala hilo.


Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho Mbunge huyo alisema kuwa tayari suala hilo wameshalizungumza na wamekubaliana kwa pamoja  kuwa watabeba mwili huo kwa kutumia gari lakini litakuwa likitembea kwa mwendo mdogo na wao bila kuwa na kelele za shamlashamla


“Naomba tuendelee kuwa na utulivu suala hili tumeshalizungumza limekwisha na tumekubaliana kuwa askario wote waliopo hapa waondoke na magari yao na siosi tutauchukua mwili wa marehemu na kuuweka kwenye gari na litatembea polepole huku na sisi tukiusindikiza kwa mguu hadi  katika kanisa la Romani Katoriki la mjini”alisema 









0 comments: