Pages

Monday, March 28, 2016

FAIDAMALI YATOA MSAADA WA BAISKELI NA KOMPUTA KWA VIKUNDI VYA WAKULIMA NA SACCOS


Mwakilishi kutoka AGRA Valentino Miheso akikabidhi Kompyuta kwa chama cha akina na mikopo (SACCOS) cha  Juhudi Ijombe Mbeya vijijini.

TAASISI  ya FaidaMali  kwa ufadhili wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani (AGRA), imetoa msaada wa baiskeli  kwa vikundi 60 vya wakulima  zenye thamani ya Sh11.4 kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano katika shughuli za kilimo kwa Wilaya tatu za Morogoro na Mbeya.


Akizungumza na vikundi vya wakulima Igurusi Wilaya ya  Mbarali Mkoani hapa Mkurugenzi wa FaidaMali  Tom Sillayo alisema  taasisi hiyo pia imetoa msaada wa komputa tano kwa vikundi vya akiba na mikopo(SACCOS)zenye thamani ya Sh5.6milioni katika Wilaya hizo tatu.

Alisema kuwa taasisi hiyo ya Faida Mali alizitaja wilaya zilizokabidhiwa  msaada huo wa baiskeli na komputa kuwa ni pamoja na Kilosa Mkoani Morogoro na Mbarali  na Mbeya vijijini ambapo imekuwa ikijishughulisha na kazi ya kutoa mafunzo kwa wakulima kwa kupitia vikundi kuhusinana na kilimo bora na cha kisasa.

“Wakulima wamekuwa wakipatiwa mafunzo juu ya mbinu mbali mbali za kilimo bora,namna ya kutumia vizuri mbolea na mbegu bora za kisasa ikiwa ni pamoja  na kujifunza namna ya kuongeza uzalishaji wa  mazao ili kuweza kupata mavuno  mengi “alisema

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi wenzake Abia Mwasuta kutoka kijiji cha Chamoto Wilaya ya Mbarali alisema wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mtaji,elimu ya ujasiliamali,vitendea kazi na ubovu wa miundombinu ya barabara.

Alisema pamoja na kupewa mafunzo na msaada wa baiskeli, wakulima wengi hawana mtaji   kwa ajili ya kumudu gharama za pembejeo  ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga na kuweza kupata mavuno mengi yatakayo wasaidia kuboresha maisha yao.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka AGRA ,Valentino Miheso alisema  mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo wakulima watapata mafunzo ya utalaam wa kilimo cha biashara,vitendea kazi na jinsi ya kuanzisha miradi midogomidogo ya ufugaji kupitia vikundi ili kuondokana na umasikini.

Alisema kuhusu komputa zinatolewa kwenye Saccos zilizopo maeneo ya vijijini ambazo vikundi vya wakulima ni wanachama na wananufaika katika kupata mikopo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kupata fedha kwa ajili ya pembejeo za kilimo.

Na Brandy Nelson,Mbeya 

0 comments: